Jumatatu, Mei 18, 2026
spot_imgspot_img

Top 5 This Week

spot_img

Related Posts

Byiringiro Lague hatamani kucheza tena katika Ligi Kuu ya Rwanda baada ya kusimamishwa na klabu ya Police FC

By Seif Shaggy Gracien Hasingizwimana,Kigali,Rwanda,
Mchezaji wa timu ya taifa ya Rwanda, Amavubi, Byiringiro Lague, ametangaza kuwa msimu huu wa mashindano utamalizika bila yeye kurejea uwanjani. Aidha, amesisitiza kuwa katika msimu ujao wa mashindano, hana mpango wa kuchezea timu yoyote ya nchini Rwanda kwa sababu anaona ligi ya hapa nchini haipo katika kiwango anachotamani.

Katika mahojiano kupitia kipindi cha Sunday Choice Live yaliyofanyika Jumapili hii, mchezaji huyo wa Police FC amesisitiza kuwa mienendo yake haiendani na mwelekeo wa soka la Rwanda kwa sasa. Amesema kuwa kutokana na malengo anayotaka kufikia katika taaluma yake, ligi ya ndani nchini haiko katika kiwango bora kwake binafsi. Maelezo haya yanakuja wakati mchezaji huyo alikuwa amesimamishwa na klabu yake ya Police FC kwa madai ya kukosa mazoezi, ingawa yeye anasema kuwa alionewa kwa sababu alikuwa mgonjwa.

Lague amesema kuwa kusimamishwa kwake kulikuja kwa ghafla kwa sababu alikuwa ametoa ripoti ya ugonjwa. Alisema: ”Walinisimamisha kwa muda usiojulikana, walinipa barua wakiniambia kuwa sishiriki mazoezi na hali nilikuwa mgonjwa. Nilikuwa nimetoa ripoti kwa madaktari wetu na viongozi nilikuwa nimewaambia kuwa mimi ni mgonjwa. Nilikuwa nimeenda hata hospitalini kutibiwa nikawaonyesha jinsi hali ilivyo, hivyo sijui ni nini kiliwapelekea kunisimamisha”.

Mbali na matatizo ya ugonjwa na mazoezi, Byiringiro Lague pia ameweka wazi matatizo yake na vyombo vya usalama barabarani kutokana na kuendesha gari akiwa amekunywa pombe. Mchezaji huyu amekiri kuwa ameshafungwa mara tatu kutokana na kosa hili, ambapo siku sita alizofungwa hivi karibuni alizitumikia katika kituo cha Polisi cha Ruyenzi.

Kuhusu mustakabali wake, mshambuliaji huyo wa pembeni amesisitiza kuwa hatachezea timu nyingine maarufu nchini Rwanda kama Rayon Sports, kwani msimu ujao anatamani kuwa nje ya Rwanda. Alisema: ”Msimu huu wa mashindano utamalizika bila mimi kucheza tena. Wazo hilo siliiingilii. Siwezi kuichezea Rayon Sports. Hakuna timu ya Rwanda ninayotaka kuichezea tena katika msimu ujao wa mashindano. Ligi ya Rwanda haipo katika kiwango ninachotaka kuchezea. Kulingana na mahali ninapotaka kufika, ligi ya Rwanda haipo katika kiwango changu binafsi”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Popular Articles